Mwanzo 41 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 41 (Swahili) Genesis 41 (English)

Ikawa, mwisho wa miaka miwili mizima, Farao akaota ndoto; na tazama, amesimama kando ya mto. Mwanzo 41:1

It happened at the end of two full years, that Pharaoh dreamed: and, behold, he stood by the river.

Na tazama, ng'ombe saba wazuri, wanono, walipanda kutoka mtoni, wakajilisha manyasini. Mwanzo 41:2

Behold, there came up out of the river seven cattle, well-favored and fat-fleshed, and they fed in the reed-grass.

Na tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda nyuma yao kutoka mtoni, wabaya, wamekonda, wakasimama karibu na wale ng'ombe wengine ukingoni mwa mto. Mwanzo 41:3

Behold, seven other cattle came up after them out of the river, ill-favored and lean-fleshed, and stood by the other cattle on the brink of the river.

Kisha hao ng'ombe wabaya waliokonda wakawala wale ng'ombe saba wazuri, wanono. Basi Farao akaamka. Mwanzo 41:4

The ill-favored and lean-fleshed cattle ate up the seven well-favored and fat cattle. So Pharaoh awoke.

Akalala, akaota ndoto mara ya pili. Tazama, masuke saba yalimea katika bua moja, makubwa, mema. Mwanzo 41:5

He slept and dreamed a second time: and, behold, seven heads of grain came up on one stalk, healthy and good.

Na tazama, masuke saba membamba, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Mwanzo 41:6

Behold, seven heads of grain, thin and blasted with the east wind, sprung up after them.

Kisha hayo masuke membamba saba yakayala yale masuke saba makubwa yaliyojaa. Basi Farao akaamka, kumbe! Ni ndoto tu. Mwanzo 41:7

The thin heads of grain swallowed up the seven healthy and full ears. Pharaoh awoke, and, behold, it was a dream.

Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo. Mwanzo 41:8

It happened in the morning that his spirit was troubled, and he sent and called for all the magicians of Egypt, and all the wise men of it. Pharaoh told them his dream, but there was no one who could interpret them to Pharaoh.

Basi mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao akisema, Nayakumbuka makosa yangu leo. Mwanzo 41:9

Then the chief cupbearer spoke to Pharaoh, saying, "I remember my faults today.

Farao aliwakasirikia watumwa wake, akanitia nifungwe nyumbani mwa mkuu wa askari, mimi na mkuu wa waokaji. Mwanzo 41:10

Pharaoh was angry with his servants, and put me in custody in the house of the captain of the guard, me and the chief baker.

Tukaota ndoto usiku mmoja, mimi na yeye; kila mtu kwa tafsiri ya ndoto yake tukaota. Mwanzo 41:11

We dreamed a dream in one night, I and he. We dreamed each man according to the interpretation of his dream.

Na huko pamoja nasi palikuwa na kijana; Mwebrania, mtumishi wa mkuu wa askari, tukamhadithia, naye akatufasiria ndoto zetu; akamfasiria kila mtu kama ilivyokuwa ndoto yake. Mwanzo 41:12

There was with us there a young man, a Hebrew, servant to the captain of the guard, and we told him, and he interpreted to us our dreams. To each man according to his dream he interpreted.

Ikawa, kama vile alivyotufasiria ndivyo ilivyotokea; mimi nalirudishwa katika kazi yangu, na yeye alitundikwa. Mwanzo 41:13

It happened, as he interpreted to us, so it was: he restored me to my office, and he hanged him."

Ndipo Farao akapeleka watu, akamwita Yusufu, wakamleta upesi kutoka gerezani. Akanyoa, akabadili nguo zake, na kuingia kwa Farao. Mwanzo 41:14

Then Pharaoh sent and called Joseph, and they brought him hastily out of the dungeon. He shaved himself, changed his clothing, and came in to Pharaoh.

Farao akamwambia Yusufu, Nimeota ndoto, wala hakuna awezaye kunifasiria; nami nimesikia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri. Mwanzo 41:15

Pharaoh said to Joseph, "I have dreamed a dream, and there is no one who can interpret it. I have heard it said of you, that when you hear a dream you can interpret it."

Yusufu akamjibu Farao, akisema, Si mimi; Mungu atampa Farao majibu ya amani. Mwanzo 41:16

Joseph answered Pharaoh, saying, "It isn't in me. God will give Pharaoh an answer of peace."

Farao akamwambia Yusufu, Katika ndoto yangu nalikuwa nikisimama ukingoni mwa mto; Mwanzo 41:17

Pharaoh spoke to Joseph, "In my dream, behold, I stood on the brink of the river:

na tazama, ng'ombe saba wanatoka mtoni, wanono, wazuri, wakajilisha manyasini. Mwanzo 41:18

and, behold, there came up out of the river seven cattle, fat-fleshed and well-favored. They fed in the reed-grass,

Kisha, tazama, ng'ombe saba wengine wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya sana, wamekonda; katika nchi yote ya Misri sijaona kama hao kwa udhaifu. Mwanzo 41:19

and, behold, seven other cattle came up after them, poor and very ill-favored and lean-fleshed, such as I never saw in all the land of Egypt for ugliness.

Na hao ng'ombe waliokonda, wabaya, wakawala wale ng'ombe saba wa kwanza, wale wanono. Mwanzo 41:20

The lean and ill-favored cattle ate up the first seven fat cattle,

Na walipokwisha kuwala haikutambulikana ya kwamba wamewala, bali wakaonekana wabaya kama kwanza. Basi nikaamka. Mwanzo 41:21

and when they had eaten them up, it couldn't be known that they had eaten them, but they were still ill-favored, as at the beginning. So I awoke.

Kisha nikaona katika ndoto yangu, na tazama, masuke saba yanatokeza katika bua moja, mema, yamejaa. Mwanzo 41:22

I saw in my dream, and, behold, seven heads of grain came up on one stalk, full and good:

Na tazama, masuke saba membamba, dhaifu, yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakatokeza baada yao. Mwanzo 41:23

and, behold, seven heads of grain, withered, thin, and blasted with the east wind, sprung up after them.

Na hayo masuke dhaifu yakameza yale masuke saba mema. Nami nikawaambia hao waganga, wala hakuna aliyeweza kunionyesha maana yake. Mwanzo 41:24

The thin heads of grain swallowed up the seven good heads of grain. I told it to the magicians; but there was no one who could explain it to me."

Yusufu akamwambia Farao, Ndoto ya Farao ni moja; Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Mwanzo 41:25

Joseph said to Pharaoh, "The dream of Pharaoh is one. What God is about to do he has declared to Pharaoh.

Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja. Mwanzo 41:26

The seven good cattle are seven years; and the seven good heads of grain are seven years. The dream is one.

Na wale ng'ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa. Mwanzo 41:27

The seven lean and ill-favored cattle that came up after them are seven years, and also the seven empty heads of grain blasted with the east wind; they will be seven years of famine.

Ndivyo nilivyomwambia Farao, ya kwamba Mungu amemwonyesha Farao atakayoyafanya hivi karibu. Mwanzo 41:28

That is the thing which I spoke to Pharaoh. What God is about to do he has shown to Pharaoh.

Tazama, miaka saba ya shibe inakuja, katika nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:29

Behold, there come seven years of great plenty throughout all the land of Egypt.

Kisha kutakuja miaka saba ya njaa baada yake; na shibe ile yote itasahauliwa katika nchi ya Misri, na njaa itaiharibu nchi. Mwanzo 41:30

There will arise after them seven years of famine, and all the plenty will be forgotten in the land of Egypt. The famine will consume the land,

Wala shibe ile haitajulikana katika nchi kwa sababu ya njaa inayokuja baadaye, maana itakuwa nzito sana. Mwanzo 41:31

and the plenty will not be known in the land by reason of that famine which follows; for it will be very grievous.

Na ndoto ya Farao kwa vile ilivyokuja mara mbili, ni kwa sababu neno hilo Mungu amelithibitisha, na Mungu atalitimiza upesi. Mwanzo 41:32

The dream was doubled to Pharaoh, because the thing is established by God, and God will shortly bring it to pass.

Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri. Mwanzo 41:33

Now therefore let Pharaoh look for a discreet and wise man, and set him over the land of Egypt.

Farao na afanye hivi, tena akaweke wasimamizi juu ya nchi, na kutwaa sehemu ya tano katika nchi ya Misri, katika miaka hii saba ya kushiba. Mwanzo 41:34

Let Pharaoh do this, and let him appoint overseers over the land, and take up the fifth part of the land of Egypt's produce in the seven plenteous years.

Na wakusanye chakula chote cha miaka hii myema ijayo, wakaweke akiba ya nafaka mkononi mwa Farao wakakilinde kuwa chakula katika miji. Mwanzo 41:35

Let them gather all the food of these good years that come, and lay up grain under the hand of Pharaoh for food in the cities, and let them keep it.

Na hicho chakula kitakuwa akiba ya nchi kwa ajili ya miaka hiyo saba ya njaa, itakayokuwa katika nchi ya Misri, nchi isiharibike kwa njaa. Mwanzo 41:36

The food will be for a store to the land against the seven years of famine, which will be in the land of Egypt; that the land not perish through the famine."

Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. Mwanzo 41:37

The thing was good in the eyes of Pharaoh, and in the eyes of all his servants.

Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? Mwanzo 41:38

Pharaoh said to his servants, "Can we find such a one as this, a man in whom is the Spirit of God?"

Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. Mwanzo 41:39

Pharaoh said to Joseph, "Because God has shown you all of this, there is none so discreet and wise as you.

Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Mwanzo 41:40

You shall be over my house, and according to your word will all my people be ruled. Only in the throne I will be greater than you."

Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:41

Pharaoh said to Joseph, "Behold, I have set you over all the land of Egypt."

Farao akavua pete yake ya muhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Mwanzo 41:42

Pharaoh took off his signet ring from his hand, and put it on Joseph's hand, and arrayed him in robes of fine linen, and put a gold chain about his neck,

Akampandisha katika gari lake la pili alilokuwa nalo. Na watu wakapiga kelele mbele yake, Pigeni magoti. Hivyo akamweka juu ya nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:43

and he made him to ride in the second chariot which he had. They cried before him, "Bow the knee!" He set him over all the land of Egypt.

Farao akamwambia Yusufu, Mimi ni Farao, na bila amri yako, mtu asiinue mkono wala mguu katika nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:44

Pharaoh said to Joseph, "I am Pharaoh, and without you shall no man lift up his hand or his foot in all the land of Egypt."

Farao akamwita Yusufu, Safenath-panea; akamwoza Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, kuwa mkewe Yusufu akaenda huko na huko katika nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:45

Pharaoh called Joseph's name Zaphenath-paneah; and he gave him Asenath, the daughter of Potiphera priest of On as a wife. Joseph went out over the land of Egypt.

Naye Yusufu alikuwa mwenye miaka thelathini, aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya uso wa Farao, akapita katika nchi yote ya Misri. Mwanzo 41:46

Joseph was thirty years old when he stood before Pharaoh king of Egypt. Joseph went out from the presence of Pharaoh, and went throughout all the land of Egypt.

Ikawa katika miaka ile saba ya shibe, nchi ikazaa kwa wingi. Mwanzo 41:47

In the seven plenteous years the earth brought forth abundantly.

Akakusanya chakula chote cha miaka ile saba katika nchi ya Misri. Akaweka chakula katika miji; chakula cha mashamba yaliyouzunguka kila mji, akakiweka ndani yake. Mwanzo 41:48

He gathered up all the food of the seven years which were in the land of Egypt, and laid up the food in the cities: the food of the field, which was round about every city, he laid up in the same.

Yusufu akakusanya nafaka kama mchanga wa pwani, nyingi mno, hata akaacha kuhesabu, maana ilikuwa haina hesabu. Mwanzo 41:49

Joseph laid up grain as the sand of the sea, very much, until he stopped counting, for it was without number.

Kabla ya kuja miaka ya njaa, Yusufu akazaliwa wana wawili, ambao Asenathi, binti Potifera, kuhani wa Oni, alimzalia. Mwanzo 41:50

To Joseph were born two sons before the year of famine came, whom Asenath, the daughter of Potiphera priest of On, bore to him.

Yusufu akamwita jina lake yule aliyezaliwa kwanza, Manase, maana alisema, Mungu amenisahaulisha taabu zangu zote, na nyumba yote ya baba yangu. Mwanzo 41:51

Joseph called the name of the firstborn Manasseh,{"Manasseh" sounds like the Hebrew for "forget."} "For," he said, "God has made me forget all my toil, and all my father's house."

Na wa pili akamwita jina lake Efraimu, maana alisema, Mungu amenipa uzazi katika nchi ya mateso yangu. Mwanzo 41:52

The name of the second, he called Ephraim{"Ephraim" sounds like the Hebrew for "twice fruitful."}: "For God has made me fruitful in the land of my affliction."

Miaka ile saba ya shibe ikaisha katika nchi ya Misri, Mwanzo 41:53

The seven years of plenty, that was in the land of Egypt, came to an end.

ikaanza kuja miaka ile saba ya njaa, kama vile Yusufu alivyosema. Kukawa na njaa katika nchi zote, bali katika nchi yote ya Misri palikuwa na chakula. Mwanzo 41:54

The seven years of famine began to come, just as Joseph had said. There was famine in all lands, but in all the land of Egypt there was bread.

Na nchi yote ya Misri ilipoona njaa, watu walimlilia Farao awape chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, Enendeni kwa Yusufu; atakavyowaambia, fanyeni. Mwanzo 41:55

When all the land of Egypt was famished, the people cried to Pharaoh for bread, and Pharaoh said to all the Egyptians, "Go to Joseph. What he says to you, do."

Njaa ikawa katika dunia yote pia. Yusufu akazifungua ghala zote, akawauzia Wamisri. Njaa ikawa nzito katika nchi ya Misri. Mwanzo 41:56

The famine was over all the surface of the earth. Joseph opened all the store-houses, and sold to the Egyptians. The famine was severe in the land of Egypt.

Watu wa nchi zote wakaja Misri kwa Yusufu; ili wanunue nafaka; kwa sababu njaa imekuwa nzito katika dunia yote.

Mwanzo 41:57

All countries came into Egypt, to Joseph, to buy grain, because the famine was severe in all the earth.