Mwanzo 48 Swahili & English

Listen/Download Audio
Mwanzo 48 (Swahili) Genesis 48 (English)

Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako hawezi; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye. Mwanzo 48:1

It happened after these things, that someone said to Joseph, "Behold, your father is sick." He took with him his two sons, Manasseh and Ephraim.

Naye akaarifiwa Yakobo ya kwamba, Angalia, mwanao Yusufu anakuja kwako. Israeli akajitia nguvu, akaketi juu ya kitanda. Mwanzo 48:2

Someone told Jacob, and said, "Behold, your son Joseph comes to you," and Israel strengthened himself, and sat on the bed.

Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki, Mwanzo 48:3

Jacob said to Joseph, "God Almighty appeared to me at Luz in the land of Canaan, and blessed me,

akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele. Mwanzo 48:4

and said to me, 'Behold, I will make you fruitful, and multiply you, and I will make of you a company of peoples, and will give this land to your seed after you for an everlasting possession.'

Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni. Mwanzo 48:5

Now your two sons, who were born to you in the land of Egypt before I came to you into Egypt, are mine; Ephraim and Manasseh, even as Reuben and Simeon, will be mine.

Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao. Mwanzo 48:6

Your issue, who you become the father of after them, will be yours. They will be called after the name of their brothers in their inheritance.

Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrathi. Nikamzika katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu. Mwanzo 48:7

As for me, when I came from Paddan, Rachel died by me in the land of Canaan in the way, when there was still some distance to come to Ephrath, and I buried her there in the way to Ephrath (the same is Bethlehem)."

Israeli akawaona wana wa Yusufu, akasema, Ni nani hawa? Mwanzo 48:8

Israel saw Joseph's sons, and said, "Who are these?"

Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki. Mwanzo 48:9

Joseph said to his father, "They are my sons, whom God has given me here." He said, "Please bring them to me, and I will bless them."

Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia. Mwanzo 48:10

Now the eyes of Israel were dim for age, so that he couldn't see. He brought them near to him; and he kissed them, and embraced them.

Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionyesha na uzao wako pia. Mwanzo 48:11

Israel said to Joseph, "I didn't think I would see your face, and, behold, God has let me see your seed also."

Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi Mwanzo 48:12

Joseph brought them out from between his knees, and he bowed himself with his face to the earth.

Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye. Mwanzo 48:13

Joseph took them both, Ephraim in his right hand toward Israel's left hand, and Manasseh in his left hand toward Israel's right hand, and brought them near to him.

Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza. Mwanzo 48:14

Israel stretched out his right hand, and laid it on Ephraim's head, who was the younger, and his left hand on Manasseh's head, guiding his hands knowingly, for Manasseh was the firstborn.

Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo, Mwanzo 48:15

He blessed Joseph, and said, "The God before whom my fathers Abraham and Isaac did walk, the God who has fed me all my life long to this day,

naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi. Mwanzo 48:16

the angel who has redeemed me from all evil, bless the lads, and let my name be named on them, and the name of my fathers Abraham and Isaac. Let them grow into a multitude in the midst of the earth."

Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase. Mwanzo 48:17

When Joseph saw that his father laid his right hand on the head of Ephraim, it displeased him. He held up his father's hand, to remove it from Ephraim's head to Manasseh's head.

Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake. Mwanzo 48:18

Joseph said to his father, "Not so, my father; for this is the firstborn; put your right hand on his head."

Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa. Mwanzo 48:19

His father refused, and said, "I know, my son, I know. He also will become a people, and he also will be great. However, his younger brother will be greater than he, and his seed will become a multitude of nations."

Akawabariki siku ile akasema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase. Mwanzo 48:20

He blessed them that day, saying, "In you will Israel bless, saying, 'God make you as Ephraim and as Manasseh'" He set Ephraim before Manasseh.

Israeli akamwambia Yusufu, Angalia, mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, naye atawarudisha mpaka nchi ya baba zenu. Mwanzo 48:21

Israel said to Joseph, "Behold, I am dying, but God will be with you, and bring you again to the land of your fathers.

Nami nimekupa wewe sehemu moja zaidi kuliko ndugu zako, niliyoitwaa katika mikono ya Waamori, kwa upanga wangu na upinde wangu. Mwanzo 48:22

Moreover I have given to you one portion above your brothers, which I took out of the hand of the Amorite with my sword and with my bow."