Zaburi 111 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 111 (Swahili) Psalms 111 (English)

Haleluya Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano. Zaburi 111:1

Praise Yah! I will give thanks to Yahweh with my whole heart, In the council of the upright, and in the congregation.

Matendo ya Bwana ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. Zaburi 111:2

Yahweh's works are great, Pondered by all those who delight in them.

Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele. Zaburi 111:3

His work is honor and majesty. His righteousness endures forever.

Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; Bwana ni mwenye fadhili na rehema. Zaburi 111:4

He has caused his wonderful works to be remembered. Yahweh is gracious and merciful.

Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele. Zaburi 111:5

He has given food to those who fear him. He always remembers his covenant.

Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. Zaburi 111:6

He has shown his people the power of his works, In giving them the heritage of the nations.

Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini, Zaburi 111:7

The works of his hands are truth and justice. All his precepts are sure.

Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili. Zaburi 111:8

They are established forever and ever. They are done in truth and uprightness.

Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa. Zaburi 111:9

He has sent redemption to his people. He has ordained his covenant forever. His name is holy and awesome!

Kumcha Bwana ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana akili njema, Sifa zake zakaa milele. Zaburi 111:10

The fear of Yahweh is the beginning of wisdom. All those who do his work have a good understanding. His praise endures forever!