Zaburi 73 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zaburi 73 (Swahili) Psalms 73 (English)

Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli, Kwa hao walio safi mioyo yao. Zaburi 73:1

> Surely God is good to Israel, To those who are pure in heart.

Nami miguu yangu ilikuwa karibu na kupotoka, Hatua zangu zilikuwa karibu na kuteleza. Zaburi 73:2

But as for me, my feet were almost gone. My steps had nearly slipped.

Maana naliwaonea wivu wenye kujivuna, Nilipoiona hali ya amani ya wasio haki. Zaburi 73:3

For I was envious of the arrogant, When I saw the prosperity of the wicked.

Maana hawana maumivu katika kufa kwao, Na mwili wao una nguvu. Zaburi 73:4

For there are no struggles in their death, But their strength is firm.

Katika taabu ya watu hawamo, Wala hawapati mapigo pamoja na wanadamu. Zaburi 73:5

They are free from burdens of men, Neither are they plagued like other men.

Hivyo kiburi kimekuwa mkufu shingoni mwao, Jeuri huwavika kama nguo. Zaburi 73:6

Therefore pride is like a chain around their neck. Violence covers them like a garment.

Macho yao hutokeza kwa kunenepa, Wameipita kadiri ya mawazo ya mioyo yao. Zaburi 73:7

Their eyes bulge with fat. Their minds pass the limits of conceit.

Hudhihaki, husimulia mabaya, Husimulia udhalimu kana kwamba wako juu. Zaburi 73:8

They scoff and speak with malice. In arrogance, they threaten oppression.

Wameweka kinywa chao mbinguni, Na ulimi wao hutanga-tanga duniani. Zaburi 73:9

They have set their mouth in the heavens. Their tongue walks through the earth.

Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao. Zaburi 73:10

Therefore their people return to them, And they drink up waters of abundance.

Nao husema, Mungu ajuaje? Yako maarifa kwake aliye juu? Zaburi 73:11

They say, "How does God know? Is there knowledge in the Most High?"

Fahamu, ndivyo walivyo wasio haki, Na kwa kustarehe sikuzote wamepata mali nyingi. Zaburi 73:12

Behold, these are the wicked. Being always at ease, they increase in riches.

Hakika nimejisafisha moyo wangu bure, Nimenawa mikono yangu kwa kutokukosa. Zaburi 73:13

Surely in vain I have cleansed my heart, And washed my hands in innocence,

Maana mchana kutwa nimepigwa, Na kuadhibiwa kila asubuhi. Zaburi 73:14

For all day long have I been plagued, And punished every morning.

Kama ningalisema, Nitasimulia kama hayo; Kumbe! Ningaliwadanganya kizazi cha wana wako. Zaburi 73:15

If I had said, "I will speak thus;" Behold, I would have betrayed the generation of your children.

Nami nalifikiri jinsi ya kufahamu hayo; Ikawa taabu machoni pangu; Zaburi 73:16

When I tried to understand this, It was too painful for me;

Hata nilipoingia katika patakatifu pa Mungu, Nikautafakari mwisho wao. Zaburi 73:17

Until I entered God's sanctuary, And considered their latter end.

Hakika Wewe huwaweka penye utelezi, Huwaangusha mpaka palipoharibika. Zaburi 73:18

Surely you set them in slippery places. You throw them down to destruction.

Namna gani wamekuwa ukiwa mara! Wametokomea na kutoweshwa kwa utisho. Zaburi 73:19

How they are suddenly destroyed! They are completely swept away with terrors.

Ee Bwana, kama ndoto wakati wa kuamka, Uondokapo utaidharau sanamu yao. Zaburi 73:20

As a dream when one wakes up, So, Lord, when you awake, you will despise their fantasies.

Moyo wangu ulipoona uchungu, Viuno vyangu viliponichoma, Zaburi 73:21

For my soul was grieved. I was embittered in my heart.

Nalikuwa kama mjinga, sijui neno; Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako. Zaburi 73:22

I was so senseless and ignorant. I was a brute beast before you.

Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume. Zaburi 73:23

Nevertheless, I am continually with you. You have held my right hand.

Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu. Zaburi 73:24

You will guide me with your counsel, And afterward receive me to glory.

Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe. Zaburi 73:25

Who do I have in heaven? There is no one on earth who I desire besides you.

Mwili wangu na moyo wangu hupunguka, Bali Mungu ni mwamba wa moyo wangu Na sehemu yangu milele. Zaburi 73:26

My flesh and my heart fails, But God is the strength of my heart and my portion forever.

Maana wajitengao nawe watapotea; Umewaangamiza wote waliokuacha Wewe. Zaburi 73:27

For, behold, those who are far from you shall perish. You have destroyed all those who are unfaithful to you.

Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote. Zaburi 73:28

But it is good for me to come close to God. I have made the Lord Yahweh my refuge, That I may tell of all your works.